10 Desemba 2014 - 10:30
Shaaban Robert Fasihi wa pekee

Shaban Robert ni mshairi, fasihi na mwandishi mahiri ambaye anamchango mkubwa katika kuendeleza tamaduni na lugha adhimu ya kiswahili, Shaaban Reobert ni fahari ya Tanzania.

Shaban Robert ni mshairi, fasihi  na mwandishi mahiri ambaye anamchango mkubwa katika kuendeleza tamaduni na lugha adhimu ya kiswahili, Shaaban Reobert ni fahari ya Tanzania.

Maisha yake

Shaaban Robert alizaliwa Januari mosi, 1909 Kijiji cha Vibambani, jirani na Machui, kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika Shule ya Msimbazi, jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1922 na 1926, alifaulu na kupata cheti. Alikuwa mshairi na mwandishi wa riwaya. Mchango wake katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa, kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na zinatumika mashuleni. Alifariki dunia Juni 22, 1962. Aliajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika Idara ya Forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu, kumesaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili. Tangu mwaka 1944 alihamia ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Mbali na maandiko yake, alikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika Languages Board. Kwa ujumla Shaaban Robert aliandika vitabu ishirini na viwili. Baadhi ya vitabu hivi ni Adili na Nduguze, Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Baada ya Miaka Hamsini, na Maisha Yangu. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina, Kiingereza na Kirusi. Alifariki dunia Juni 22, 1962 na kuzikwa Machui. Aliacha wake watatu na watoto kumi.

Kazi alizofanya alipokuwa karani wa serikali

Akiwa serikalini alifanya kazi forodhani Pangani na mahali pengine tangu mwaka 1926 hadi 1944; Idara ya Wanyama tangu mwaka 1944 hadi 1946; na Ofisi ya Mkuu wa Jimbo la Tanga tangu mwaka 1946 hadi 1952. Sehemu zingine ni Ofisi ya Kupima Nchi Tanga, tangu mwaka 1952 hadi 1960. Alipandishwa cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka 1929, na mwaka 1944 alipandishwa tena kuwa Grade II Local Service. Alikuwa mwanachama wa East African Swahili Committee, East African Literature Bureau, Tanganyika Languages, Tanga Township Authority.

Baadhi ya mashairi ya Shaaban Robert.

Kazi bora Afrika, yenye cheo na heshima

Yapaswa kukumbuka, kuni ukulima

Vibaya kuzohalika,kushika jembe kulima.

 

...watu wengi wa asili, walikuwa wakulima

Ubora wa jambo hili, yapaswa kuutazama

Isipotee asili, makabila yakazama

Ukulima ni halali, siyo kazi ya lawama.

Shaaban Robert pia alikuwa ni mtetezi wa heshima na haki za wanawake:

Si wajibu kusema, mke hana fadhili

Wapo waume si wema, tia katika akili

Na mabaya yanauma, hapana wa kuhimili

Ukivunja heshima, mke naye hunakili.

 

...ningojeni kina mama, mimi nitawatetea

Tawatetea lawama, la ovyo lisilo njia

Litaondoka lazima,kwa upesi kukimbia

Mwisho mtajaliwa, nanyi mpewe heshima.

 

Shaaban Robert pia alikuw ni mwalimu wa Tabia na maadili mema:

Ambapo anatuambia kuwa thamani ya mtu ni maadili mema si utajiri, nguvu wala ufahari;

 

Wapo watu maskini, hawana cha kutumia

Lakini wana thamani,kwa ubora wa tabia

Watu hao duniani, ni chumvi ya kutumia

Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

 

Wapo wenye milki, watakavyo hutumia

Lakini si marafiki, kwa ubaya wa tabia

Hao hawachukuliki,hatari kukaribia

Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

 

Kifo na kumbukumbu

Marehemu Shaaban Robert alifariki Tanga Juni 22, 1962, alizikwa Machui, Tanga. Alituzwa zawadi ya waandishi inayojulikana kama ‘Margaret Wrong Memorial Prize’na nishani ya M.B.E.

Mungu ilaze roho ya Shaaban Robert mahala pema peponi.

Tags